Kiswahili

Kiswahili

Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.

1 Wakorintho 2:9

English

Je, kanisa la ID (ID church) ni kanisa gani? Kanisa la ID lilianzishwa Uppsala, Sweden. Tumeendelea kukua taratibu na kutekeleza wito wetu. Tunaamini ya kwamba Mungu hajawasahau watu wa Ulaya na wa Afrika pia, na anataka kutenda jambo jema na la ajabu ndani ya maisha yetu.

Kusudi letu ni kujenga kanisa ambalo linamtukuza Mungu, na kuhudumia watu wake. Tunaamini ya kwamba maombi, biblia, neno la uzima, nyimbo na kuabudu vyote kwa pamoja vina nafasi kubwa katika kutimiza lengo hili. Tunaamini katika kauli mbiu yetu isemayo: Imani Halisi, Jamii ya Kweli.

Hivyo basi, kwanini usishiriki na sisi jumapili hii katika ibada, mafundisho na fellowship mnamo saa 4 asubuhi na saa 10 jioni pale Mbalizi, Mlowo, Iyunga na Songwe, Tanzania.

Tuna imani wachungaji wetu watakukaribisha na kukufanya ujisikie nyumbani!

Karibu!

WasilIana Nasi

    wpChatIcon